Alikubali kuishi karibu na wakwe baadaye akalazimika kwenda mbali nao

Swali: Nilikubaliana na baba wa mke wangu kwamba baada ya ndoa nitaishi karibu nao, lakini baada ya ndoa nikalazimika kuishi mbali nao katika nchi nyingine. Kutokana na hali ya maisha na kazi yangu, mke wangu alikubali kuhamia pamoja nami, lakini baba yake anakataa sana. Je, kwa hali hii ninakuwa nimevunja ahadi na kuwa na dhambi ilihali mke wangu hana pingamizi?

Jibu: Ikiwa mke wako ameridhia, basi hakuna ubaya kumhamisha ukae naye. Ama ikiwa hakuridhia, basi waislamu wanapaswa kushikamana na masharti yao. Lakini ikiwa ameridhia, basi una haki ya kuhamia naye, na si halali kwa mama yake wala baba yake kumzuia katika hilo. Kwa sababu unaweza kuwa unamhitaji na hivyo hakuna ubaya. Ama ikiwa yuko kwa wazazi wake na anataka kutimiza sharti lile, basi ni juu yako kulitekeleza sharti hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Waislamu wako juu ya masharti yao.”[1]

”Hakika masharti yenye haki zaidi kutimizwa ni yale ambayo kwayo mmehalalishiwa tupu.”[2]

[1] at-Tirmidhiy (1352).

[2] al-Bukhaariy (2721) na Muslim (1418).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/41)
  • Imechapishwa: 18/03/2026