Swali: Lau mume na mke watatofautiana kuhusu kwenda mahala, mwanamke anasema ni lazima aende sokoni wakati mume anakataa hilo. Wakavutana na mwishowe kukatoe Talaka. Ni nani ambaye anapata madhambi katika suala hili?

Jibu: Mwanamke ndiye anapata madhambi. Kwa kuwa ni wajibu kwake kumtii mume. Asitoke isipokuwa kwa idhini yake. Hii ni haki ya mume juu yake ya kwamba asitoke nyumbani kwake isipokuwa kwa idhini yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14301
  • Imechapishwa: 17/11/2014