al-Waadi´iy ndoa ya wanandoa wawili ambapo mmoja anaswali na mwingine haswali

Mwenye kuacha swalah anazingatiwa ni kafiri. Haijuzu kwako kumuoza msichana wako, dada yako au nduguyo. Kama ambavo haijuzu kwa mwenye kuswali kumuoa mwanamke ambaye haswali. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema katika Kitabu Chake kitukufu:

وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ

”Wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa.” (60:10)

فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Mkiwatambua kuwa ni waumini, basi msiwarejeshe kwa makafiri; wao si wake halali kwao na wala wao waume hawahalaliki kwao.” (60:10)

Vilevile mwenye kuacha swalah harithi na wala harithiwi. Kwa sababu anahesabika ni kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muislamu hamrithi kafiri na wala kafiri hamrithi muislamu.”

“Watu wenye dini mbili hawarithiani.”

Au Hadiyth yenye manaa kama hiyo.

Kwa hali yoyote anatakiwa kutaamiliwa muamala wa kafiri. Haya ndio maoni sahihi katika madhehebu ya wanachuoni. Pia ndio maoni ya Imaam Ahmad bin Hanbal. Kadhalika ndio maoni yaliyotiwa nguvu na Haafidhw Ibn-ul-Qayyim katika kitabu chake “as-Swalaah” na kabla yake Haafidhw Muhammad bin Naswr al-Marwaziy katika kitabu chake “Ta´dhwiym Qadr-is-Swalaah”.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 38
  • Imechapishwa: 04/04/2020