al-Waadi´iy kuhusu talaka tatu kwa mpigo

Swali: Mtu akimtaliki mke wake mara tatu katika kikao kimoja inahesabika ni talaka tatu au moja?

Jibu: Inahesabiwa ni talaka moja. Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesema:

“Talaka tatu zilikuwa zinahesabiwa ni talaka moja wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakati wa Abu Bakr na wakati wa ´Umar.”

Kuna kipindi ´Umar alikuwa anaona  kuwa zote tatu zinapita. Hata hivyo Sunnah ya Mtume wa Allaah wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ina haki zaidi ya kufuatwa. ash-Shawkaaniy amesema:

“Maimamu wanne wamechukua maoni ya ´Umar. Ikiwa mmeacha Sunnah kwa ajili yake ´Umar, anaangukia wapi masikini huyu mbele ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Ikiwa mnaiacha Sunnah kwa ajili ya madhehebu, ni yenye kudharauliwa zaidi kuliko kuyapinganisha na Sunnah za Mtume wa Allaah wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?”[1]

[1] Nayl-ul-Awtwaar.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 296
  • Imechapishwa: 09/08/2025