Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak na dawa ya meno wakati ambapo mtu amefunga katika Ramadhaan?
Jibu: Ni sawa kutumia Siwaak ya Salvadora persica[1] ikiwa ni msafi.
Kuhusiana na dawa ya meno, ninashauri kutoitumia wakati wa Ramadhaan. Hata hivyo sina dalili yoyote ya kwamba inaharibu swawm. Ni wajibu kuwa makini ili kusiwe na chochote kitachoingia tumboni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kutilia umuhimu mkubwa wa kupandisha maji puani ikiwa mtu si mwenye kufunga. Kwa sababu mfungaji yuko katika khatari ya kupata maji ndani ya tumbo.
[1] http://en.wikipedia.org/wiki/Salvadora_persica
- Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 78-79
- Imechapishwa: 26/08/2020
Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak na dawa ya meno wakati ambapo mtu amefunga katika Ramadhaan?
Jibu: Ni sawa kutumia Siwaak ya Salvadora persica[1] ikiwa ni msafi.
Kuhusiana na dawa ya meno, ninashauri kutoitumia wakati wa Ramadhaan. Hata hivyo sina dalili yoyote ya kwamba inaharibu swawm. Ni wajibu kuwa makini ili kusiwe na chochote kitachoingia tumboni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kutilia umuhimu mkubwa wa kupandisha maji puani ikiwa mtu si mwenye kufunga. Kwa sababu mfungaji yuko katika khatari ya kupata maji ndani ya tumbo.
[1] http://en.wikipedia.org/wiki/Salvadora_persica
Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 78-79
Imechapishwa: 26/08/2020
https://firqatunnajia.com/al-waadiiy-kuhusu-siwaak-na-dawa-ya-meno-wakati-wa-funga/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)