Swali: Ni ipi hukumu ya kuwachukua picha wanachuoni katika mikutano na mihadhara yao? Ni picha hizi zilizoruhusiwa?
Jibu: Picha ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Malaika hawaingii katika nyumba ilio na mbwa wala picha.”
Amesema tena:
“Allaah amewalaani watengeneza picha.”
Katika “Jaamiy” ya at-Tirmidhiy kupitia Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Shingo itatoka Motoni siku ya Qiyaamah. [Shingo hiyo] itakuwa na macho mawili yenye kuona, masikio yenye kusikia na ulimi wenye kuongea na utasema: “Mimi nimepewa kazi kwa watu aina tatu: kila jabari mkaidi, kila mwenye kuomba mungu mwengine pamoja na Allaah na wale watengeneza picha.”
Siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataa kuingia chumba cha ´Aaishah kwa sababu alikuwa amefunika kwa pazia chumba chake cha hazina ambacho kilikuwa na picha. Hii ni dalili dhidi ya wale wanaosema kwamba picha zilizoharamishwa ni zile za viwiliviwili [vya watu na wanyama]. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataa kuingia chumbani mpaka ilipopasuliwa ile pazia kisha akasema:
“Hakika miongoni mwa watu wataopata adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale wenye kutengeneza picha hizi.”
Picha ambazo hazina budi kama mfano wa picha za leseni, picha za pasipoti na picha za kitambulisho basi dhambi ziko kwa serikali.
- Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, 26
- Imechapishwa: 20/12/2019

Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, 26
Imechapishwa: 20/12/2019
https://firqatunnajia.com/al-waadiiy-kuhusu-kwamba-rekodi-za-video-ni-katika-picha-pia/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)