al-Madkhaliy kuhusu Muhammad Mukhtaar ash-Shanqiytwiy

Swali: Ndugu mmoja ametupa kanda ya Sharh ´Umdat-ul-Ahkaam cha Shaykh Muhammad [al-Mukhtaar] ash-Shanqiytwiy na una kaseti 400. Tuache ibaki Msikitini?

Jibu: Mtu mtu huyu, mimi sijasoma Sharh hii. Sijui. Nimeambiwa kuwa mtu huyu hawezi kupambanua baina ya Ahaadiyth Swahiyh na Dhaifu, na kwamba anatangamana na Hizbiyuun na Sufiyyuun nawala hana mawasiliano na Ahl-us-Sunnah. Ndio maana siwezi kuzitakasa wala kumtakasa mtu huyu. Kwa kuwa sijazisoma. Nanyi hamna haja… Ni nani anaesambaza kanda ya mtu huyu? Sio Ahl-us-Sunnah wanaosambaza kanda zake. Wanaozisambaza ni Hizbiyyuun. Yeye mwenyewe hajionyeshi kuwa ana vikundi vikundi. Lakini wakati unapoona watu hawa wamemzunguka na kanda zake na wanamchukulia kuwa Imaam wa Waislamu, ni dalili ionyeshayo kuwa mtu huyu ni katika wao. Ni njia ya khatari inayowafanya vijana kuwa vikundi vikundi. Mko na vitabu vya Salaf. Vinawatosheleza.Fiqh ya Salaf inawatosheleza. Kwa kuwa hayo yatakuja kuwapeleka katika mambo mengine.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=Pknjz6e_fEo
  • Imechapishwa: 28/07/2020