Swali 216: Je, katika mjeledi “Dhwilaal-ul-Qur-aan” ya Sayyid Qutwub ndani yake kuna mashaka upande wa ´Aqiydah?

Jibu: Bali imejaa mambo yanayopingana na ´Aqiydah. Mtu huyo – Allaah amrehemu na tunamuomba Allaah awarehemu maiti wote wa Kiislamu – sio katika wanachuoni. Ni miongoni mwa watu waliosoma al-Madiynah na watu waliosoma adabu…

Kuhusu kitabu chake hakifundishi ´Aqiydah, hakithibitishi hukumu na hakitegemewi katika mfano wa hayo. Haitakikani kwa mwanafunzi aliyeanza na ambaye amekulia kwenye njia ya elimu kukichukulia ni miongoni mwa vitabu vya elimu ambacho atakitegemea. Elimu ina vitabu vyake na wanaume wake.

Namnasihi mwanafunzi kusoma vitabu vya wanachuoni wa kale; maimamu wane, Taabi´uuun, watu wa haki, wanachuoni wa Uislamu wenye kutambulika kuwa na ´Aqiydah iliosalimika, lukuki ya elimu, uhakiki na kubainisha malengo ya Shari´ah. Nao – na himdi zote njema anastahiki Allaah – ni wengi. Vitabu vyao – himdi zote njema anastahiki Allaah – vimehifadhiwa. Chimbuko cha yote hayo – kuyapima maneno ya watu –  yanapimwa kwa kuyaweka kwenye Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yote hayo – himdi zote njema anastahiki Allaah – yameandikwa kwenye vitabu “as-Swahiyh” na “as-Sunan” vya wanachuoni na vitabu vya mapokezi kama vile vya “al-Muswannaf” na mfano wake. Kwa hivyo mwanafunzi hana udhuru kwa kufanya mapungufu. Haisihi vitabu vya waliokuja nyuma vikafanywa ni vyenye kuvihukumu vitabu vya waliotangulia.

Muulizaji: Vipi mwanafunzi mwenye kukaa na Ahl-us-Sunnah na Ahl-ul-Bid´ah na anasema:

“Inatosha kwa Umma kufarikiana. Mimi nakaa na wote”?

Jibu: Huyu ni mzushi. Hakutenganisha kati ya haki na batili na anadai eti kufanya hivo ni kuleta umoja. Mtu huyo ni mtu wa Bid´ah. Tunamuomba Allaah amwongoze.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 440-441
  • Imechapishwa: 03/04/2020