Swali: Nimewasikia baadhi ya wanafunzi wanasema kuwa tafsiyr ya Shaykh [´Abdur-Rahmaan] as-Sa´diy (Rahimahu Allaah) ni tafsiyr isiyokuwa ya kisomi. Je, maneno yake ni sahihi?

Jibu: Huyu hajui tafsiyr na wala hajui lolote. Tafsiyr ya Shaykh as-Sa´diy ni ya kielimu na usulubu wake ni mwepesi. Ni tafsiyr iliyo muntazi na nzuri. Ndani yake mna maneno ya wanachuoni wawili; Ibn Taymiyyah na Ibn-ul-Qayyim na khaswa katika mambo ya Tawhiyd na ´Aqiydah. Ni tafsiyr nzuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (45) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-4-20.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020