al-Fawzaan kuhusu shirki ndogo haisamehewi

Swali: Umetaja kwamba wanachuoni wametofautiana juu ya suala la kwamba shirki ndogo inasamehewa au haisamehewi. Ni maoni yepi yaliyo na nguvu?

Jibu: Maoni yaliyo na nguvu ni kwamba haisamehewi kutokana na kuenea kwa Aayah. Lakini hata hivyo haidumishi Motoni milele kama ambavo atadumishwa Motoni milele yule ambaye yuko na shirki kubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 56
  • Imechapishwa: 08/07/2018