al-Fawzaan kuhusu kuuza na kujitolea viungo kumpa mgonjwa

Swali: Ni ipi hukumu ya kuuza na kupeana viungo kumpa [mgojwa] aliye hai au kutoa kwa maiti?

Jibu: Kwanza kuuza viungo haijuzu. Ni haramu.

Pili kuchukua viungo kutoka kwa maiti haijuzu. Ana heshima yake.

“Kuvunja mkono wa maiti ni kama kumvunja akiwa hai.”

Maiti ana heshima yake. Haijuzu kuchukua kitu kutoka kwenye viungo vya maiti.

Kuhusiana na kuchukua kiungo kutoka kwa aliye hai na kumpa mgonjwa kwa ajili ya kutaka kumuokoa, kutokana na kauli sahihi ni kwamba ikiwa kama haimdhuru kitu yule mwenye kujitolea kufanya hivo na ikawa itamsaidia yule mgonjwa, na mtoaji akawa ni mtu ameshabaleghe na ana akili, ni sawa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020