al-Fawzaan kuhusu kifo cha Mtume na kuswaliwa swalah ya jeneza

Swali: Nimetatizwa na suala la kwamba shahidi haswaliwi kwa kuwa shahaadah ni uombezi na shahidi amesamehewa dhambi zake kwa shahaadah. Kwa nini Maswahabah walimswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilihali amesamehewa aliyotanguliza na aliyochelewesha?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mauti yake hayasifiwi kuwa ni shahaadah. Isipokuwa juu ya kauli inayosema kuwa alikufa kwa sababu ya sumu. Hii ni shahaadah isiyomzuia kuswaliwa. Kama tulivosema kwamba mwenye kufa kwa kuungua na moto, kuzama, ugonjwa wa tumbo n.k., hawa ni mashahidi Aakhirah na wanafanyiwa katika jeneza wanayofanyiwa wengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufa uwanjani. Ikiwa ni shahidi basi ni shahidi maalum.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-29.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014