al-Fawzaan kuhusu hukumu ya kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa

Udhhiyah ni jambo limependekezwa. Ni kichinjwa kinachochinjwa kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah katika siku ya ´Iyd-ul-Adhwhaa na masiku ya Tashriyq. Hivyo mtu anakuwa amemwigiliza Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi Allaah alipomwamrisha kumchinja mwanae Ismaa´iyl kwa ajili ya kumpa mtihani na majaribio. Wakati Ibraahiym alipoazimia kutekeleza amri ya Allaah, ndipo Allaah akafuta hukumu hii na akamkomboa kwa kichinjwa kitukufu hali ya kuwa ni fidia juu ya Ismaa´iyl (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ibraahiym akachinja na hivyo kitendo hichi kikawa kimesuniwa mpaka siku ya Qiyaamah.

Vivyo hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichinja kondoo dume wawili wenye pembe kwa ajili ya kuhuisha Sunnah ya Ibraahiym. Aliwawekea Ummah wake Shari´ah hiyo. Hata hivyo si jambo la wajibu. Bali ni jambo limependekezwa mno kwa mujibu wa jopo la wanachuoni wengi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mukhtaswar (2/584)
  • Imechapishwa: 12/07/2020