Swali: Kuna watu ambao wanaeneza kwenye intaneti ya kwamba wewe unatahadharisha waangushaji ambao wanaudhoofisha Uislamu na mmoja wao amesema ni Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy. Ni ipi Radd yako kwa watu hawa ambao wanawazushia uongo maulamaa na wanachuoni? Unawanasihi nini wanafunzi ambao wanaeneza maneno kama haya?

Jibu: Nasaha yangu kwa wanafunzi nawausia kutafuta elimu na waachane na mambo haya. Wasiyaingilie. Wasiseme fulani amesema hivi na vile, sawa kwenye intaneti na kwengine. Wajishughulishe na kutafuta elimu na kutaka kuijua haki na kuitendea kazi. Waachane na maneno ya watu na kumtia huyu makosani na yule kwenye usawa. Haya hayawahusu. Kinachowahusu ni kutafuta haki, kutaka kuijua haki na kuitendea kazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14763
  • Imechapishwa: 21/06/2020