Swali: Wako ambao wanasema kwamba maoni ya Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika imani ni yaleyale kama ya Murji-ah. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) ni mwanachuoni, Muhaddith na Faqiyh, hata kama alikuwa mwenye nguvu zaidi katika Hadiyth kuliko Fiqh.

Sijui kuwa ana maoni yenye kufahamisha juu ya Irjaa´. Lakini wanaotaka kuwakufurisha watu husema juu yake na kwa watu mfano wake kwamba ni Murji-ah. Inahusiana na kupeana majina bandia. Mimi nashuhudia juu ya Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) juu ya kuwa na msimamo, ´Aqiydah salama na makusudio mazuri.

Lakini pamoja na hivyo sisemi kuwa hakosei. Kwa sababu hakuna yeyote, baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amekingwa na kukosea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-As-ilah al-Qatwariyyah, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 16/02/2019