Nilimwambia daktari [Rabiy´ al-Madkhaliy] – na bado ninaonelea hivi na ninafikiria kuwa waandishi wengi na wanachuoni wetu wanaonelea hivi – ya kwamba watu wengi wanaonelea kuwa ni vigumu kukubali haki:

إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا

”Hakika Sisi Tutaweka juu yako kauli nzito.” (73:05)

Pale ambapo haki ukiongezea juu yake inapokutana na ukali na ugumu, hapo uzito aina mbili unakuwa umekutana. Hilo linawashtua watu na Da´wah ya haki. Lengo la Da´wah ni kuwafanya wawe katika haki. Hakuna mwanafunzi yeyote katika sisi ambaye hakuhifadhi Aayah katika Qur-aan na Ahaadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo zinahimiza upole na ulaini. Aayah zinajulikana na hatuna haja ya kuzitaja. Kwa mfano Allaah (´Azza wa Jall) alimuamrisha Muusa na ndugu yake Haaruun (´alayhimaas-Salaam) pale Aliposema:

اذْهَبَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ

“Nendeni kwa Fir’awn, hakika yeye amepindukia mipaka. Mwambieni maneno laini, huenda akawaidhika au akaingiwa na khofu.” (20:43-44)

Vovyote ambavyo mtu atakavokuwa mpotevu, sifikirii kuwa kuna Muislamu anaonelea kuwa anamkaribia Fir´awn ambaye alitumiwa Muusa na Haaruun. Pamoja na hivyo Allaah Aliwaamrisha Mitume hawa wawili watukufu na Manabii walioteuliwa kuzungumza kwa upole na muasi mkubwa kwenye ardhi aliyesema:

أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ

“Mimi ni mola wenu mkuu.” (79:24)

Ninaonelea kuwa Sayyid Qutwub sio kama Fir´awn kabisa. Anaporaddiwa lengo ni wafuasi wake leo. Kwa sababu yeye kishakufa. Kwa vile wanaolengwa ni wale waliohai, mimi nitasema juu yao yale niliyosema kwa huyu ambaye kishakufa; shari yao haikifii shari ya Fir´awn ambaye alidai uungu. Kwa ajili hiyo ninaonelea kuwa haitakikani kukusanya kati ya ugumu aina mbili. Moja wapo ni lazima nako ni kule kulinganizi kwa haki kunakotofautisha kati ya haki na batili na mtu na ndugu yake. Ndio maana mingoni mwa majina ya Qur-aan tukufu ni “al-Furqaan” na miongoni ma majina ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaitwa “al-Faariq”. Kwa sababu alitofautisha kati ya haki na batili, Tawhiyd na shirki, baba na mtoto wake, mtoto na baba yake na kadhalika. Namna hii ndivyo inavokuwa ulinganizi juu ya haki. Inatosheleza kwetu kuwalingania watu katika Da´wah hii kutokana na Kauli Yake (Ta´ala):

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ

“Waite [watu] katika njia ya Mola Wako kwa hikmah na mawaidha mazuri.” (16:125)

Inaweza kuwa vizuri kutaja kitu kama ukumbusho na kujisalimisha na Kauli ya Mola Wetu katika Qur-aan:

وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ

“Na kumbusha, kwani hakika ukumbusho [mawaidha] unawafaa Waumini.” (51:55)

Myahudi, kafiri na mtu mwenye chuki aliyekuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamsalimia Salaam ya: “Kifo kiwe juu yako, ewe Mtume wa Allaah!”

Alichojibu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni:

“Na wewe pia.”

Hata hivyo ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye alikuwa nyuma ya pazia akakasirika na kusema:

“Kifo, laana na khasira iwe juu yako, ewe ndugu wa tumbili na nguruwe!”

Wakati myahudi yule alipotoka Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkataza ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na kumwambia:

“Katu hakukuwi upole kwenye kitu isipokuwa hukipamba na katu haukosi kwenye kitu isipokuwa hukifanya kikawa kibaya.”

Hivyo akawa amebainisha udhuru wake na kadhalika ni jambo liko na kila mwenye hamasa na Da´wah na kutumia kitu katika ukali:

“Je, hukusikia nilivosema?”

Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hukusikia na mimi nilivosema?”

Amesema: “Kifo kiwe juu yako” na mimi nikasema “Na wewe pia” mambo kwisha. Da´wah inatakiwa kuwa pasina ugumu huu kwa sababu hauleti kheri yoyote.

Uhakika wa mambo ni kwamba mimi nafurahia sana harakati za kielimu za ndugu yetu [Rabiy´ al-Madkhaliy], lakini ninamnasihi atumie upole kwa watu hawa ambao wamepinda na Da´wah ya haki kwa sababu ya Da´wah ya mtu mjinga. Nilisema kuwa daktari Sayyid Qutwub hakuwa ni mwanachuoni na pengine hazingatiwi kuwa hata katika wanafunzi. Hiyo ndio hali ya waandishi wengi wengine na khaswa watu wa Misri. Wanaandika na huku wanafikiria kuwa wanafanya mambo mzuri. Haya ndio maoni yangu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (915)
  • Imechapishwa: 26/08/2020