Akisujudu msomaji nawe Sujuud, na si venginevyo

Swali: Nikipita kwenye Aayah ya sujuud wakati niko nasoma Qur-aan katika ufosini yangu au niko nawasomesha wanafunzi au mahali pengine kokote – je, nisujudu sijda ya kisomo au hapana? Je, Sujuud ni ya kwa ajili ya msomaji na msikilizaji?

Jibu: Sujuud ya kisomo imependekezwa kwa msomaji na msikilizaji. Sio lazima. Haikusuniwa kwa msikilizaji isipokuwa amfuate msomaji. Akisujudu msomaji basi msikilizaji naye atasujudu. Akisoma Aayah ya kisomo ofisini mwake au katika hali ya masomo basi imesuniwa kwako kusujudu. Aidha imesuniwa kwa wanafunzi kusujudu pamoja nawe. Kwa sababu ni wenye kusikia. Ni sawa pia ukiacha kusujudu. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Zayd bin Thaabit ya kwamba alisoma mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Suurah “an-Najm” na hakusujudu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumkemea. Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Hiyo ni dalili inayojulisha kuwa Sujuud ya kisomo sio lazima na kwamba imesuniwa kwa msikilizaji kusujudu pale ambapo atasujudu msomaji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/411)
  • Imechapishwa: 12/11/2021