Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka hina juu ya kichwa chenye mvi?
Jibu: Sunnah ni yeye kubadilisha kichwa na ndevu zinapokuwa na mvi. Katika hali hiyo mtu azibadilishe kwa rangi isiyokuwa nyeusi. Azibadilishe kwa rangi kama ya njano, nyekundu au rangi baina ya nyeusi na nyekundu. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoona kichwa na ndevu zake Abu Quhaafah, ambaye alikuwa ni baba yake Abu as-Swiddiyq, ambazo zilikuwa nyeupe kama kivimbe akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Zibadilishe mvi hizi… ”
Kwa maana ya nywele za kichwa na ndevu vyote viwili.
”… na jiepushe na [rangi] nyeusi.”
Swali: Vipi kuhusu masharubu?
Jibu: Hukumu ni moja. Zinafanywa kama ndevu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24541/حكم-تغيير-شيب-الراس-والشارب-بالحناء
- Imechapishwa: 26/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)