Swali: Msichana mdogo ambaye amevaa Hijaab na ambaye ameshikamana na vazi la Kiislamu lililowekwa katika Shari´ah na anausitiri mwili wake mzima isipokuwa uso na viganja vya mikono. Je, anaruhusiwa akitaka kuswali kila nyakati ya swalah msikitini kufanya hivo? Je, anaruhusiwa daima kwenda na mume wake?
Jibu: Hapana vibaya kwa mwanamke kuswali msikitini akiwa ni mwenye kujisitiri Hijaab inayokubalika katika Shari´ah na hali ya kuwa amefunika uso wake, viganja vyake vya mikono na mwili wake mzima. Sambamba na hayo ajiepushe na manukato na kuonyesha mapambo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah.”
Lakini bora ni yeye kuswali nyumbani kwake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“… na nyumba zao ni bora kwao.”[1]
[1] Ahmad (5211) na Abu Daawuud (480).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/80)
- Imechapishwa: 20/11/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
10. Swalah ya mwanamke inapoonekana miguu au nywele zake
Swali 10: Wanawake wengi wanachukulia wepesi katika jambo la swalah ambapo inaonekana mikono yao au sehemu yake na vivyo hivyo nyayo zao na pengine baadhi ya miundi yao. Je, swalah yake ni sahihi katika kipindi hicho? Jibu: Ni lazima kwa mwanamke muungwana na ambaye ´ibaadah ni yenye kumuwajibikia kufunika mwili…
In "1. Sharti za swalah"
Kuchukulia wepesi wanawake kufunika mikono na miguu katika swalah
Swali: Wanawake wengi wanachukulia wepesi katika swalah zao ambapo inaonekana mikono yao au sehemu yake na vivyo hivyo miguu yake. Je, kipindi hicho swalah inasihi? Jibu: Ni lazima kwa mwanamke muungwana ambaye ´ibaadah ni zenye kumuwajibikia kufunika mwili wake mzima ndani ya swalah usipokuwa uso na viganja vya mikono. Kwa…
In "Swalah ya mwanamke"
04. Mavazi sahihi anayotakiwa mwanamke kwenda kuswali nayo ´iyd
Kutokana na yale tuliyonukuu, imepata kubainika kuwa waandishi hawa wanaonelea kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa wasichana kutoka kwenda katika uwanja. Yahifadhi haya. Huenda ikafika siku waandishi hawa kwa sababu ya hasadi na chuki wakapinga yale ambayo siku moja walikuwa wakiyakubali pale watapoona wanusuraji wa Sunnah ni wenye kuitendea…
In "Swalaat-ul-´Iydayn - al-Albaaniy"