Swalah ya mkusanyiko inakuwa pamoja na imamu mteule peke yake?

Swali: Unasemaje juu ya ambaye anasema kuwa swalah ya mkusanyiko inakuwa na yule imamu mteule peke yake?

Jibu: Maoni haya hayana msingi wenye kutegemewa. Lakini lililo la wajibu ni kukimbilia kuswali pamoja na yule imamu mteule na kutochelewa. Lakini pale ambapo Allaah atakadiria kuchelewa kutokana na sababu miongoni mwa sababu kisha akakutana na ambaye ataswali pamoja naye, basi kunatarajiwa kwao thawabu za mkusanyiko kutokana na kuenea kwa dalili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/81)
  • Imechapishwa: 20/11/2021