Akiba chache isiyotosheleza matumizi iwapo watahiji nayo

Swali: Mimi ni mwanamke ambaye sijatekeleza faradhi ya hajj mpaka hivi sasa. Mwaka huu mume wangu ana pesa ambazo tunaweza kuhiji kwazo. Lakini mali hii ndio akiba yetu yote. Tukihiji kwayo basi tutakuwa na upungufu wa kipesa. Mume wangu ni mwajiriwa.

Jibu: Subirini mpaka mwaka ujao huenda Allaah akakufungulieni riziki na mkaweza kuhiji. Ama kwa hivi sasa, midhali mali mlionayo endapo mtahiji nayo basi mtakuwa na upungufu katika matumizi na mahitajio mengine, basi hajj haikulazimuni.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/970
  • Imechapishwa: 16/12/2018