Ajifanyie hajj ya kujitolea au amuhijie bibi yake?

Swali: Kuna mtu anataka kujifanyia hajj inayopendeza na mama yake anamtaka kumfanyia hajj bibi yake ambaye kishakufa. Je, bora ni kujifanyia hajj mwenyewe au amtii mama yake katika kumuhijia bibi yake?

Jibu: Amtii mama yake na amhijie bibi yake. Anabashiriwa kheri. Anatarajiwa kuwa na thawabu za hajj.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23776/حكم-من-امرته-امه-بالحج-عن-جدته-المتوفاة
  • Imechapishwa: 26/04/2024