Kususa kumegawanyika sehemu mbili:

1- Kususa kwa ajili ya dini. Hili ni jambo lina hukumu zake maalum. Kidhibiti chake ni kwamba inajuzu kumsusa muislamu kwa ajili ya Allaah ikiwa katika kufanya hivo kuna manufaa. Hili ni kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivowasusa wahalifu watatu katika vita vya Tabuuk na mfano wa hayo.

2- Kususa kwa ajili ya mambo ya kidunia. Mtu kumsusa ndugu yake muislamu kwa ajili amemuudhi, ameingiwa na chuki moyoni n.k. Kumsusa mtu ikiwa inahusina na jambo la kidunia anaweza kumsusa ndugu yake kwa siku tatu. Ni haramu kumsusa zaidi ya siku tatu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 485
  • Imechapishwa: 10/05/2020