Umesema kwenye barua yako:
“Hivyo basi, mimi ninakunasihi, ee Shaykh, kuchunga ulimi wako na kumzungumza vibaya mtu huyu ambaye Allaah amenufisha kupitia yeye.”
Hii ni nasaha nzuri lau ingeliwekwa mahala pake stahiki. Ni zawadi yenye thamani kwa yule anayetaka kuihifadhi dini yake. Lakini unaninasihi nisitoe nasaha. Je, hii ni nasaha? Hii ni njia ya kurudisha kheri na kuzuia kutokamana na njia ya Allaah.
Mche Allaah, ee Shaykh ´Abdullaah, na rejea katika haki. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba sina chembe ya shaka kwa niliyofanya. Bali uhakika wa mambo naonelea kuwa ni wajibu wangu. Ninajua mengi ya kutosha juu ya mtu huyu na mfumo wake ili inistahikie kuwanasihi wengine na kubainisha ni makosa yepi yanayopatikana katika mfumo huu. Ninafanya hivo ikiwa ni nasaha kwa wanafunzi walioghurika nao na ili kutekeleza haki ya Allaah kutetea Uislamu na Tawhiyd kama ambavo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni kipi kilicho na haki zaidi kutetewa? Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi, ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, au heshima ya Hasan al-Bannaa. Allaah hakuamrisha kuwapiga vita washirikina na makafiri kwa ajili ya ´Aqiydah sahihi? Allaah (Ta´ala) amesema:
وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ
“Na piganeni nao mpaka kusiweko fitina na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah pekee.”[1]
Fitina imefasiriwa kuwa ni shirki. Allaah hakuhalalisha kuwaua makafiri na wanawake na watoto wao kuwafanya mateka na mali zao kuzifanya ni ngawira kwa waislamu kwa ajili ya ´Aqiydah? Je, haki ya mtu imeharamishwa kuvunjwa akifanya shirki kubwa na kukubaliana na matendo yao na akazusha katika dini Bid´ah na akaweka Shari´ah mambo yasiyokuwepo? Imeharamishwa kuvunjwa ikiwa mtu anataka kuwabainshia haki watu waliodanganywa na mtu huyu na mfumo wake? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba wajibu nilio nao mimi, wewe na wanafunzi wengine wote, ni kuinusuru dini kutangulizwe juu ya mambo mengine yote katika ardhi ili kumtii Allaah, kutimiza haki Yake, kuinusuru dini Yake na kuihifadhi ´Aqiydah ya waislamu.
[1] 02:193
- Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Radd-ul-Jawaab, uk. 33-34
- Imechapishwa: 05/07/2020

Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Radd-ul-Jawaab, uk. 33-34
Imechapishwa: 05/07/2020
https://firqatunnajia.com/ahmad-an-najmiy-anamjibu-ibn-jibriyn-11/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)