as-Safaariyniy amesema:

“Ahl-us-Sunnah ni makundi matatu: Athariyyah linaloongozwa na Ahmad bin Hanbal, Ashaa´irah linaloongozwa na Abul-Hasan al-Ash´ariy na Maaturiydiyyah linaloongozwa na Abu Mansuur al-Maaturiydiy. Ama kuhusiana na makundi potofu, ni mengi sana.”[1]

Kuwagawa Ahl-us-Sunnah katika makundi matatu ni jambo linatakiwa kujadiliwa. Ahl-us-Sunnah pasi na shaka yoyote ni kundi moja ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amelieleza kwa kusema:

“Ni mkusanyiko.”

Katika upokezi mwingine amesema:

“Ni lile litakalofuata yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

au:

“Ni lile litakalofuata yale ninayofuata mimi na Maswahabah zangu.”

Mtu anapata kufahamu kwamba ni wenye kuafikiana juu yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Kwa hivyo ni kundi moja. Mwandishi mwenyewe (Rahimahu Allaah) amesema katika utangulizi wa shairi lake wakati alipotaja Hadiyth hii:

“Maandiko haya hayalihusu kundi lingine isipokuwa Ahl-ul-Athar.”[2]

Bi maana Athariyyah. Hivyo basi mtu anapata kufahamu kuwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kundi moja, nalo ni Athariyyah – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] Lawaamiy´-ul-Anwaar al-Bahiyyah (1/73).

[2] Abu Daawuud (4596) na at-Tirmidhiy (2641) kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Mishkaah” (171).

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan Abaa Butwayn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haashiyah ´alaa Lawaamiy´-il-Anwaar al-Bahiyyah (1/73)
  • Imechapishwa: 06/03/2019