Swali: Hakika unajua kueneza kwa njia mbalimbali za mawasiliano leo. Kuna ambao wanatumia njia hizi ili kueneza fitina kati ya watu na kutahadharisha wanachuoni na watawala. Ni ipi hukumu ya watu hawa?
Jibu: Tahadharini nao na mtahadharishe nao. Watu hawa ni wajibu kwenu kutahadhari nao na kutahadharisha nao na shari yao. Watu hawa wameanguka na himdi zote ni za Allaah. Hawasadikishwi, maneno yao hayakubaliwi na wala hawana taathira yoyote katika jamii. Utaona ndio watu waliio na hadhi ya chini kabisa na ndio watu wenye kudharauliwa kabisa katika jamii.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14759
- Imechapishwa: 28/06/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Tahadharini nao na tahadharisheni nao
Swali: Ni ipi hukumu ya makosa ya baadhi ya watawala au wanachuoni yanayoenezwa kwenye intaneti ambayo hayazidishi chochote katika kuitengeneza jamii ya Kiislamu isipokuwa maovu zaidi na kuleta tofauti na khaswa leo? Jibu: Mnajua kuwa walinganizi wa fitina na wa upotevu lengo leo ni kutaka kufarikisha waislamu na kubatilisha hukumu…
In "al-Fawzaan kuhusu kutahadharisha Ahl-ul-Bid´ah"
20. Uwajibu wa kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah na kutowanyamazia
Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema: 9- Tambua kupinda kutoka katika Njia iliyonyooka ni kwa namna mbili. Wa kwanza ni mtu ameteleza akapinda na Njia, pamoja na kuwa hakukusudia isipokuwa kheri. Kosa lake lisichukuliwe kama kiigizo, kwa sababu ni mwenye kuangamia. Mwingine, ameenda kinyume na haki na yale wachaji Allaah waliyokuwemo…
In "al-Fawzaan kuhusu kutahadharisha Ahl-ul-Bid´ah"
Wanatahadharisha fataawaa za wanachuoni
https://youtu.be/I9OD7KQlcn8 Swali: Kuna baadhi ya waswidi ambao wanaona kwamba kueneza na kusambaza fataawaa za wanachuoni wetu kama zinazohusu Fiqh na mfumo zilizotolewa na mfano wa Ibn Baaz, al-Albaaniy, Ibn ´Uthaymiyn na al-Fawzaan kwamba ni upumbavu na ujinga na kwamba ni sababu ya kufarikiana kwa vijana. Unasemaje juu ya hilo pamoja…
In "Msimamo juu ya wanachuoni na fataawaa zao"