Afadhali mjinga kuliko huyu…

Swali: Una nasaha yoyote kumpa mwanafunzi ambaye hakusoma kwa wanachuoni na badala yake aliwatembelea tu na akanunua baadhi ya vitabu ili kufaidika navyo na utamuona anatoa Fatwa katika kila kitu hata katika mambo makubwa na anamtia kasoro yule asiyemuuliza?

Jibu. Hili halijuzu. Huku ni kuzungumza juu ya Allaah bila ya elimu.

Elimu haipatikani kwa kusoma vitabu wala kwa kuwatembelea wanachuoni, kama anavyosema. Elimu inapatikana kwa kuitafuta, kwa muda mrefu, uvumilivu katika kusoma na kuuliza juu ya yenye kutatiza. Hivi ndivyo elimu inavyotafutwa. Kuna taasisi za kielimu, masomo na vyuo vikuu vimewekwa kwa ajili ya kutafuta elimu. Vilevile katika mizunguko ya misikitini kwa wanachuoni wa waislamu. Ambaye anataka kutafuta elimu apite njia hii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameseama:

“Mwenye kuchukua njia akitafuta elimu ndani yake… “

Tazama alivyosema:

“Mwenye kuchukua njia… “

Sio kukaa na kuanza kusoma na kujifanya mwanachuoni na kuanza kutoa Fatwa na kujibebesha mambo makubwa ilihali ni mjinga. Bali afadhali mjinga kuliko huyu. Kwa kuwa mjinga anajijua kuwa ni mjinga na wala haingilii mambo ya Fataawaa.  Ama huyu anajidai kuwa ana elimu na anafikiri kuwa amekuwa mwanachuoni! Matokeo yake anajiletea madhara kwenye nafsi yake na kwa waislamu.

Ni wajibu kwa mtu huyu kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14759
  • Imechapishwa: 28/06/2020