“Ahadi ya kingereza au ya kiarabu”

Miongoni mwa maneno ya kipumbavu ya wapumbavu huku kwetu ni pale unapomuahidi unamsikia anakuuliza “hii ni ahadi ya kingereza au ni ahadi ya kiarabu.” Kwa msemo mwingine anataka kusema kuwa wangereza ndio wenye kutimiza ahadi. Bila ya shaka huu ni upumbavu na kughurika na makafiri hawa. Ni kweli kuwa kuna wangereza waumini na waislamu, lakini wengi wao ni makafiri. Kutimiza kwao kwa ahadi hawafanyi hivo kwa ajili ya Allaah. Wanafanya hivo kwa manufaa yao kwa watu.

Muumini ni yule anayetimiza ahadi. Akitimiza ahadi basi huyo ni muumini na akienda kinyume [na alichoahidi] basi ana chembe za unafiki.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/470)
  • Imechapishwa: 01/09/2025