Swali: Watu wengi wanajengea hoja kwa kunyamaza kwa Ahl-us-Sunnah wengi wakati wa kuenea kwa Bid´ah na matamanio, na khaswa hii leo, na kunapotokea ukaripiaji inakuwa pasi na upazaji sauti wa wanazuoni na kuzungumza hilo kwa uwazi. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Si sahihi. Ahl-us-Sunnah wote hawanyamazi. Ni lazima Allaah afanye kuwepo mtu katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah anayekemea. Pengine wakawa si wengi. Anaweza kuwa ambaye anafanya hivo ni mmoja tu; Allaah anamfanya kuwasimamishia hoja waja Wake. Si kweli kusema kuwa wananyamaza kabisa. Hawanyamazi wote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tatwhiyr-il-I´tiqaad (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/et–1432-05-15.mp3
  • Imechapishwa: 12/11/2022