Afanye nini mtu ambaye amehisi kutokwa na kitu kwenye tupu?

Swali: Mimi nasumbuliwa juu ya kutokuwa na uhakika wa kutokwa na madhiy. Wakati ninapokuwa na fikira za matamanivu sijui kama nimetokwa nayo au hapana. Je, kuna kidhibiti juu ya kutoka kwake?

Jibu: Mimi nitampa muulizaji na wasikilizaji kidhibiti chenye manufaa kilicho na dalili kutoka katika Sunnah. Ukiwa na mashaka ya kutokwa na upepo, mkojo, madhiu au kitu kingine ambacho kinachengua wudhuu´, basi msingi ni utwahara na usafi. Dalili ya hilo ni kwamba Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walimstahikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba wakati mwingine mtu anahisi tumboni mwake kitu na wakati huohuo hana uhakika kama ametokwa na kitu au hapana. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Asitoke mpaka asikie sauti au ahisi harufu yake.”

Kwa msemo mwingine mpaka awe na uhakika.

Kwa hiyo jambo lina wasaa. Lakini wako watu ambao wasiwasi unawazidi na wanapokuwa na mashaka, wanapoingiwa na mashaka tu basi kwa mfano wanaenda kutazama kichwa cha dhakari. Hakuna haja ya kufanya hivo. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema:

“Anapoingiwa na mashaka mmoja wenu basi ahakikishe na atazame.”

Bali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Asitoke [ndani ya swalah] mpaka asikie sauti au ahisi harufu yake.”

Midhali masuala yanahusiana na kuwa na shaka, basi usifungue na wala usitazame. Tunajaribu kulisahau na kulipuuzia. Msingi ni utwahara na usafi bado uko palepale.

Vivyo hivyo wako watu wengine ambao wanahisi unyevunyevu kwenye tupu ya nyuma na hawajui kama ni jasho au ni kitu kilichotoka. Tuseme nini? Tuseme kuwa msingi ni utwahara na usafi au tuseme kuwa ni msingi ni unajisi? Msingi ni unajisi na kwamba ni jasho. Khaswakhaswa ikiwa mtu anahisi hivo katika masiku ya joto na linapotea katika masiku ya baridi. Hicho ni kiashirio cha wazi juu ya kwamba ni joto na msingi ni usafi na utwahara.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1224
  • Imechapishwa: 09/09/2019