Swali: Kuna mtu alijiunga na imamu ambaye alikuwa anaswali swalah ya kupatwa kwa jua na mtu huyo akidhani kuwa ni swalah ya faradhi. Mswaliji huyu afanye nini?
Jibu: Haya ndio tuliyotaja punde kidogo[1]. Ameingia akadhani kuwa imamu anaswali swalah ya faradhi. Kisha wakati imamu aliposimama baada ya Rukuu´ ya kwanza na akaanza tena kusoma Qur-aan ndipo akatambua kuwa ni swalah ya kupatwa kwa jua. Afanye nini? Akitenge na imamu na akamilishe faradhi. Kwa sababu amejiunga kwa kujengea kwamba ni faradhi na hivyo anatakiwa kuikamilisha. Anatakiwa kujitenga na imamu kwa sababu hawezi kumfuata imamu kwa kuwa imamu atarukuu´ mara mbili kwenye Rak´ah moja, jambo ambalo halisihi katika swalah ya faradhi. Pale tu utakapojua kuwa ni swalah ya kupatwa kwa jua basi unatakiwa kujitenga na kuswali kivyako na ukamilishe swalah yako ya faradhi kwa sababu ndivyo ulivyonuia kuanzia mwanzoni mwa swalah. Kisha baada ya hapo ujiunge na imamu katika zile Rak´ah zitazokuwa zimebaki katika swalah ya kupatwa kwa jua.
[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kuanzwe-swalah-ya-faradhi-au-swalah-ya-kupatwa-kwa-jua/
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (72) http://binothaimeen.net/content/1649
- Imechapishwa: 05/04/2020
Swali: Kuna mtu alijiunga na imamu ambaye alikuwa anaswali swalah ya kupatwa kwa jua na mtu huyo akidhani kuwa ni swalah ya faradhi. Mswaliji huyu afanye nini?
Jibu: Haya ndio tuliyotaja punde kidogo[1]. Ameingia akadhani kuwa imamu anaswali swalah ya faradhi. Kisha wakati imamu aliposimama baada ya Rukuu´ ya kwanza na akaanza tena kusoma Qur-aan ndipo akatambua kuwa ni swalah ya kupatwa kwa jua. Afanye nini? Akitenge na imamu na akamilishe faradhi. Kwa sababu amejiunga kwa kujengea kwamba ni faradhi na hivyo anatakiwa kuikamilisha. Anatakiwa kujitenga na imamu kwa sababu hawezi kumfuata imamu kwa kuwa imamu atarukuu´ mara mbili kwenye Rak´ah moja, jambo ambalo halisihi katika swalah ya faradhi. Pale tu utakapojua kuwa ni swalah ya kupatwa kwa jua basi unatakiwa kujitenga na kuswali kivyako na ukamilishe swalah yako ya faradhi kwa sababu ndivyo ulivyonuia kuanzia mwanzoni mwa swalah. Kisha baada ya hapo ujiunge na imamu katika zile Rak´ah zitazokuwa zimebaki katika swalah ya kupatwa kwa jua.
[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kuanzwe-swalah-ya-faradhi-au-swalah-ya-kupatwa-kwa-jua/
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (72) http://binothaimeen.net/content/1649
Imechapishwa: 05/04/2020
https://firqatunnajia.com/afanye-nini-mswaliji-aliyebainikiwa-kuwa-imamu-anaswali-swalah-ya-kupatwa-kwa-jua/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)