Swali: Je, kusimamisha adhabu za Kishari´ah hufuta madhambi kama vile kuua, kupigwa mawe, kupigwa mijeledi na mfano wa hayo?
Jibu: Ndiyo. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alipotaja madhambi alisema:
”Yeyote ambaye Allaah apata adhabu yake hapa duniani, basi hiyo huwa ni kafara kwake.”
Ikiwa mtu alipigwa mijeledi kisha hakurudia tena uzinzi, basi hiyo inakuwa kafara kwake. Ikiwa alizini kisha akapigwa mawe kwa kuwa aliwahi kuingia ndani ya ndoa, basi hiyo inakuwa ni tawbah kwake na Allaah humfutia dhambi yake kwa sababu hiyo. Hatashitakiwa nayo siku ya Qiyaamah, kwani Allaah hamkusanyii adhabu mbili; adhabu ya duniani na adhabu ya Aakhirah. Lakini mzinifu aliyepigwa mijeledi, akasimamiwa adhabu, kisha akarudia tena kwenye uzinzi, basi atachukuliwa kwa uzinzi wa pili, si kwa ile mara ya kwanza. Hivyo ndivyo ilivyo katika kila dhambi; dhambi ya kwanza ambayo alitubia au akasimamiwa adhabu yake, basi hatochukuliwa hatua tena.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2247/الحدود-كفارة-للذنوب
- Imechapishwa: 15/03/2026
Swali: Je, kusimamisha adhabu za Kishari´ah hufuta madhambi kama vile kuua, kupigwa mawe, kupigwa mijeledi na mfano wa hayo?
Jibu: Ndiyo. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alipotaja madhambi alisema:
”Yeyote ambaye Allaah apata adhabu yake hapa duniani, basi hiyo huwa ni kafara kwake.”
Ikiwa mtu alipigwa mijeledi kisha hakurudia tena uzinzi, basi hiyo inakuwa kafara kwake. Ikiwa alizini kisha akapigwa mawe kwa kuwa aliwahi kuingia ndani ya ndoa, basi hiyo inakuwa ni tawbah kwake na Allaah humfutia dhambi yake kwa sababu hiyo. Hatashitakiwa nayo siku ya Qiyaamah, kwani Allaah hamkusanyii adhabu mbili; adhabu ya duniani na adhabu ya Aakhirah. Lakini mzinifu aliyepigwa mijeledi, akasimamiwa adhabu, kisha akarudia tena kwenye uzinzi, basi atachukuliwa kwa uzinzi wa pili, si kwa ile mara ya kwanza. Hivyo ndivyo ilivyo katika kila dhambi; dhambi ya kwanza ambayo alitubia au akasimamiwa adhabu yake, basi hatochukuliwa hatua tena.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2247/الحدود-كفارة-للذنوب
Imechapishwa: 15/03/2026
https://firqatunnajia.com/adhabu-za-kidini-ni-kafara-ya-madhambi/