Abu Ishaaq al-Huwayniy ataamiliwe kama Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Ni yapi maoni yenu juu ya Muhaddith Abu Ishaaq al-Huwayniy na kitabu “Taysiyr ´Uluum-ul-Hadiyth”?

Jibu: Ni jambo lenye kujulikana kwamba Abu Ishaaq ana elimu katika Hadiyth. Ana uelewa na elimu kuhusu Takhriyj katika Hadiyth.

Hata hivyo kumepokelewa kutoka kwake mambo mengi yanayoenda kinyume na madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hivyo inatakiwa kutaamiliana naye mu´amala wa Ahl-ul-Bid´ah. Kuna watu wenye kutosheleza katika Ahl-ul-Bid´ah ambao ni wajuzi katika Takhriyj. Hakuna haja yake. Ni katika mfumo wa Salaf-us-Swaalih mwanafunzi ajiepushe na kuongeza idadi ya Ahl-ul-Bid´ah, kuwapa mshangilio, kuwapa nguvu na kurejea katika vitabu vyao na kuchuma faida humo. Kunaweza kutokea hilo. Yale ambayo Ahl-us-Sunnah wameandika katika Takhriyj na Mustwalah yanatosheleza kwa kurejea katika vitabu vya Abu Ishaaq.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin ´Umar Baazmuul
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rapidshare.com/files/336359028/Bazmul_Huw.wav.html
  • Imechapishwa: 22/04/2015