Swali: Je, hukumu za ki-Fiqh zichukuliwe kutoka katika madhehebu ya Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) au yaachwe kwa kuzingatia ya kwamba madhehebu yake yamesimama juu ya rai na si dalili na lingine ni kwa kuzingatia ya kwamba ametuhumiwa kuwa yuko na Irjaa´.

Jibu: Enyi ndugu, waacheni maimamu na msiwaponde! Abu Haniyfah ni katika maimu wakubwa. Ni imamu aliyetangulia miongoni mwa maimamu wane. Ni katika waliokuja baada ya Taabi´uun. Baadhi ya maimamu wanasema ni katika Taabi´uun kwa kuwa alikutana na Maswahabah. Lakini kauli sahihi ni kwamba hakukutana na Maswahabah bali alikutana na Taabi´uun. Ni katika waliokuja baada ya Taabi´uun (Rahimahu Allaah). Ni mwanachuoni wa Fiqh. Fiqh ndio uelewa wa Qur-aan na Sunnah. Ni imamu mtukufu.

Hata hivyo, yeye na wengine ni Mujtahiduun. Wanapatia na kukosea wakati mwingine. Kunachukuliwa Ijtihaad na Fiqh yao yale yanayoafikiana na dalili, sawa Abu Haniyfah na wengine. Hili si kwa Abu Haniyfah peke yake.

Mwenye kusema kuwa ana Irjaa´ kuna faida gani ya kupekua mambo haya kwa imamu mtukufu kama huyu miongoni mwa maimamu wa Waislamu?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (37) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-1-25.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020