3Kisha, Sarai akampa Abrahamu Hagari, mjakazi wake ambaye alikuwa Mmisri, awe mke wake. Haya yalitokea baada ya Abrahamu kukaa katika nchi ya Kanaani kwa muda wa miaka kumi. 4Abrahamu akamchukua Hagari, naye Hagari akapata mimba. Lakini mara tu alipoona amepata mimba, Hagari akaanza kumdharau bimkubwa wake. 5Sarai akamwambia Abrahamu: “Wewe utawajibika kwa ubaya ninaotendewa. Mimi nilikupa mjakazi wangu, lakini alipopata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake! Mwenyezi Mungu na ahukumu kati yako na mimi!” 6Lakini Abrahamu akamwambia Sarai: “Mjakazi wako yuko chini ya mamlaka yako; mfanyie upendavyo.” Basi, Sarai akamtesa Hagari mpaka akatoroka.
- Marejeo: Mwanzo 16:03-06
- Imechapishwa: 03/02/2020

Marejeo: Mwanzo 16:03-06
Imechapishwa: 03/02/2020
https://firqatunnajia.com/abrahamu-na-wakeze-wawili-katika-biblia/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)