Swali: Nimesikia baadhi ya walinganizi wakisema inajuzu kuwa na kipingamizi kwa Allaah, Uislamu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na anasema tuache watu wachague dini na waabudu wapendacho. Na anataka waondoshe adhabu ya kuritadi na anataka kuachwe kujengwe kanisa katika miji ya Waislamu. Ipi Radd yako shaykh?
Jibu: Sijui maneno haya wayasemayo wanayasema kwa akili na dini au upumbavu na maradhi ya nyoyo. Je, haya yanatokwa na mtu aliyekosa imani au kwa mtu asiyejua alisemalo? Vipi tuwe na kipingamizi kwa Allaah? Allaah (Jalla wa ´Alaa) Katuamrishakumtii na kumtii Mtume Wake:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَطِيعُواْ اللّهَ وَأَطِيعُواْ الرَّسُولَ
”Enyi mlioamini! Mtiini Allaah, na mtiini Mtume.” (04:59)
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَطِيعُواْ اللّهَ وَرَسُولَهُ وَلاَ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَأَنتُمْ تَسْمَعُونَ
”Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na Mtume wake, wala msijiepushe naye, nanyi mnasikia.” (08:20)
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا
“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha.” (04:65)
Akiwa na kipingamizi kwa Allaah akikusudia kukataa maneno ya Allaah na Sunnah ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kupa kipaumbele rai na matamanio kabla ya Kitabu na Sunnah, ni upotofu na inaweza kumfanya mtu akaritadi. Tunawajibika kuamini.
آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللّهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ
”Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola Wake na waumini vile vile. Wote wamemuamini Allaah na Malaika Wake na Vitabu vyake na Mitume Wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume Wake na husema: “Tumesikia na tumetii. Tunakutaka maghfira Mola Wetu! Na marejeo ni Kwako”.” (02:285)
Haya maneno yana uchafu kama kipingamizi kwa Allaah na Mtume Wake, au uhuru wa dini!! Dini zote zimefutwa baada ya Allaah Kumtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Shari´ah yake imekhatimu Shari´ah zote za kabla na kufuta dini zingine zote. Ikawa ni wajibu kwa viumbe vyote kumtii Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kufuata Sunnah zake. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hatosikia yeyote kuhusu mimi si myahudi wala mnaswara kisha asiniamini isipokuwa ataingia Motoni.”
Kwa kuwa Muhammad ndiyo Mtume na Nabii wa mwisho. Tunaamini Mitume wote waliotangulia na Risalah zao. Lakini ´amali na utekelezaji ni kwa mujibu wa Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=129316
- Imechapishwa: 28/07/2020

Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=129316
Imechapishwa: 28/07/2020
https://firqatunnajia.com/abdul-aziyz-aalush-shaykh-kuhusu-kauli-ya-as-suwaydaan-uhuru-wa-dini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)