´Abaa´ah ndo Jilbaab iliyotajwa katika Qur-aan. Kwa ajili hiyo ndio maana Ameamrisha mtu kujumuisha kati ya Khimaar na Jilbaab juu ya Khimaar. Hili ni kwa sababu ´Abaa´ah iko wazi kwa mbele. Kwa hivyo Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ

“Ee Nabii! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao.” (33:59)

Wakati wa Jaahiliyyah wanawake walikuwa wakitoka na Jilbaab kichwani na wakati huo huo nusu ya kichwa kiko wazi. Baadhi ya wanawake Iraaq wanavaa vivyohivyo na kanchiri na shingo zao ziko wazi. Hivyo Allaah (´Azza wa Jall) akawafunza wanawake wa Kiislamu:

يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ

“… wajiteremshie jilbaab zao.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (101)
  • Imechapishwa: 09/04/2015