Aayah mbili za al-Baqarah zitamtosheleza anayezisoma usiku


Swali: Imepokelewa katika Hadiyth kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayesoma Aayah mbili katika Suurah al-Baqarah usiku basi zitamtosheleza.”[1]

Mtu kwa mfano akizisoma katika swalah ya Maghrib zitamtosheleza?

Jibu: Bora mtu azisome baada ya swalah ya Maghrib au baada ya adhaana ya Maghrib. Lakini akizisoma ndani ya swalah basi anatakiwa azisome kwa nia isiyokuwa hii.

Neno “zitamtosheleza” imesemekana kuwa maana yake ni kwamba zitamtosheleza kutokamana na kila baya na pia imesemekana kwamba maana yake ni kuwa zitamtosheleza juu ya kusimama usiku kuswali.

[1] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (09/94) na Muslim (01/554). Tazama https://firqatunnajia.com/28-adhkaar-wakati-wa-kulala/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 07/09/2020