Swali 99: Wako wenye kuona pindi ummah unapofikwa na janga au mtihani basi wanaitisha migomo na maandamano dhidi ya watawala na wanazuoni ili maombi yao yaweze kusikizwa. Unasemaje kuhusu njia hizi?

Jibu: Madhara hayaondoshwi kwa madhara mengine. Kukitokea tukio lenye madhara au maovu basi halitakiwi kutatuliwa kwa maandamano, migomo au uharibifu. Huu ndio ufumbuzi. Huku ni kuzidisha shari. Ufumbuzi ni kuwasiliana na wahusika na kuwanasihi na kuwabainishia lililo la wajibu juu yao pengine wakayaondosha madhara haya. Ima waliondoshe na la sivyo wananchi wanatakiwa kufanya subira kwa ajili ya kuepusha madhara makubwa zaidi kuliko.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 234
  • Imechapishwa: 07/08/2024
  • Taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy