´Aliy. Yeye ni Abul-Hasan ´Aliy bin Abiy Twaalib. Jina la Abu Twaalib ni ´Abd Manaaf bin ´Abdil-Muttwalib. Yeye ndiye kijana wa kwanza kuingia katika Uislamu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa bendera siku ya Khaybar ambapo Allaah akawapa ushindi kupitia mikono yake. Alishika uongozi baada ya kuuliwa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Hivyo akawa ni khaliyfah anayezingatiwa kwa mujibu wa Shari´ah. Aliendelea kuongoza mpaka alipouliza hali ya kuwa shahidi katika Ramadhaan mwaka wa 40 H akiwa na miaka ya 63.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 141
  • Imechapishwa: 14/12/2022