96. Athar ”Allaah kumswalia ni msamaha Wake… ”

97 – Muhammad bin Abiy Bakr ametuhadithia vivyo hivyo: Muhammad bin Sawaa’ ametuhadithia: Juwaybir ametuhadithia, kutoka kwa adh-Dhwahhaak, aliyesema kuhusiana na Aayah:

هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ لِيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا

“Yeye ndiye anakusifuni na Malaika Wake wanamuomba akughufurieni na akurehemuni ili akutoeni kutoka katika viza kuingia katika nuru; Naye ni Mwenye kurehemu waumini.”[1]

”Allaah kumswalia ni msamaha Wake na Malaika kumswalia ni du´aa.”[2]

[1] 33:43

[2] Cheni ya wapokezi ni dhaifu sana kama iliotangulia.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 83
  • Imechapishwa: 14/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy