96. Anayekufuru kwa kukusudia ni mbaya zaidi kuliko anayekufuru kwa mzaha

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ya kwanza ni maneno Yake (Ta´ala):

لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Msitoe udhuru, mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (09:66)

Ukishaelewa ya kwamba baadhi ya Maswahabah ambao walipigana vita wakiwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikufuru kwa sababu ya maneno ambayo waliyatamka kwa njia ya utani na mzaha, hapo ndipo itakubainikia ya kwamba yule mwenye kutamka neno la kufuru na akalifanyia kazi kwa kuogopa mali yake isipungue au cheo au kwa sababu anataka kumpaka mafuta mtu, ni baya zaidi kuliko yule ambaye kuongea kwa maneno ambayo anafanya nayo mzaha.

MAELEZO

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesisitiza kuzitafakari Aayah mbili katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall). Aayah ya kwanza ni maneno Yake (Ta´ala):

لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Msitoe udhuru, mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”

Aayah hii iliteremshwa juu ya wanafiki waliomtukana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake.

Anachomaanisha mtunzi (Rahimahu Allaah) ni kwamba ikiwa hawa wanafiki ambao walipigana vita bega kwa bega pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika vita vya Tabuuk walikufuru kwa neno moja walilolisema kwa njia ya mashkhara. Mtu asemeje juu ya yule ambaye anakufuru kikweli? Moyo wake ni wenye kiu juu ya hilo ili asije kupoteza nafasi, hadhi yake na mfano wa hayo? Hili ni baya na khatari zaidi. Uhakika wa mambo ni kwamba wote wamekufuru, ni mamoja ikiwa wamefanya hivo kwa njia ya mzaha au kukusudia kweli, kufuru, woga au matarajio. Kila ambaye atadhihirisha Uislamu na akaficha kufuru ni mnafiki, pasi na kujali vyovyote itakavyopitika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 103
  • Imechapishwa: 28/11/2023