Maneno yake Shaykh:

“Naamini kwamba kila kilichozuliwa katika dini ni Bid´ah.”

Tofauti na wale wenye kusema kwamba yapo mambo yaliyozuliwa ndani ya dini ambayo ni mazuri. Bali kila kilichozuliwa ndani ya dini ni Bid´ah. Haya yamechukuliwa kutoka katika Hadiyth:

“Kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”

Kuhusu mambo ya kiada kama mfano wa mavazi, makazi na vipando ni miongoni mwa vitu vilivyoumbwa na Allaah na sio Bid´ah. Watu wa kale walikuwa hawapandi gari na sisi tunazipanda kwa sababu ni miongoni mwa vitu alivyotuhalalishia Allaah. Amesema (Ta´ala):

قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ

“Sema: “Nani aliyeharamisha mapambo ya Allaah ambayo amewatolea waja Wake na vizuri katika riziki?”[1]

Mambo ya kimavazi, makazi, vipando na ya mashamba vyote hivi ni katika vitu visivyoingia ndani ya ´ibaadah. Bali tunavitumia katika ´ibaadah na tunasaidika kwavyo juu ya ´ibaadah. Tunapanda gari kwa ajili ya kwenda hajj, tunapanda gari kwa ajili ya kwenda kutafuta elimu, tunapanda gari kwa ajili ya kwenda Jihaad, tunatumia vipaza sauti kwa ajili ya kutoa Khutbah na mihadhara na vinatusaidia katika kufanya ´ibaadah. Kwa sababu ni miongoni mwa vitu alivyotuhalalishia Allaah. Sio Bid´ah. Ni miongoni mwa vitu ambavyo Allaah ametuumbia:

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا

“Yeye ndiye ambaye amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini.”[2]

Msingi juu ya vitu hivi ni uhalali. Kuhusu msingi wa ´ibaadah ni kujizuia isipokuwa mpaka kwa dalili. Kuhusu katika mambo ya kawaida, mavazi, vipando, vyakula na vinywaji msingi wake ni uhalali isipokuwa vile vilivyofahamishwa na dalili juu ya uharamu wake.

[1] 07:32

[2] 02:29

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 133-134
  • Imechapishwa: 01/06/2021