95. Kaburi linatakiwa kumfanya mtu awe na bidii ya ´ibaadah na matendo mema

Mja akitafakari kwa uoni wake na kuona kuwa atatumbukia kwenye shimo hili na kupata yale aliyoyachuma hapo ndipo atatilia umuhimu mkubwa katika ´ibaadah na kukithirisha matendo mema. Anatakiwa kutambua kuwa matendo yake wataonyeshwa ndugu zake maiti.

Abud-Daraa´ alikuwa akisema:

“Ee Allaah! Najilinda Kwako kufanya matendo ambayo nitaaibika nayo kwa ´Abdullaah bin Rawaahah.”

Tunaomba ulinzi kwa Allaah kuabika kati ya ndugu wema na wachaji. Tunaomba ulinzi kwa Allaah kufedheheka pindi tutaposimama kwa Yule mwadilifu wa kuhukumu mbele ya walimwengu. Tunamuomba Allaah atuwafikishe kwa yale anayoyapenda na kuyaridhia. Mujaahid amesema:

“Muumini hupata bishara njema ya wema wa mtoto wake baada ya kufa kwake ili aweze kufurahi.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 205
  • Imechapishwa: 07/12/2016