94. Mwenye kutendea kazi Tawhiyd pasi na kuielewa wala kuiamini ni mnafiki

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Akiifanyia kazi Tawhiyd bila ya kuifahamu na wala haiamini ndani ya moyo wake, ni mnafiki na ni [mtu wa] shari kuliko kafiri wa asili kabisa. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ

“Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika Moto.” (04:145)

MAELEZO

Hili ni jambo la wazi kuhusiana na yule mwenye kuijua haki na akaichukia kwa moyo wake kwa ukaidi. Haifungulii kifua na wala haikubali. Hata hivyo anaonyesha kuwa anafuata Shari´ah ili kutaka kumpaka mchanga wa macho Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waumini.

Kuhusiana na yule asiyefahamu kabisa lakini akawa anatenda kama wanavyotenda wengine pasi na kuelewa kile kitu wanachofanya na ni yapi madhumuni yake, lililo la wajibu ni yeye kuitafuta haki na kujifunza. Akiendelea kupinga kwa moyo, huyo ni mnafiki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 102
  • Imechapishwa: 28/11/2023