Murji-ah wameyaondosha matendo katika imani na maana yake. Wamegawanyika mafungu mbalimbali:

1 – Karraamiyyah. Wanasema kuwa imani ni kutamka kwa ulimi peke yake.

2 – Ashaa´irah. Wanasema kuwa imani ni kuamini kwa moyo peke yake.

3 – Murji-ah al-Fuqahaa. Wanasema kuwa imani ni kuamini kwa moyo na kutamka kwa ulimi peke yake. Wanayaondosha matendo katika imani.

4 – Jahmiyyah, nao ndio waovu zaidi. Wanasema kuwa imani kule kutambua ndani ya moyo peke yake hata kama mtu hatoamini.

Wote wameafikiana juu ya kwamba matendo hayaingii katika imani. Ndio maana wakaitwa “Murji-ah”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 72
  • Imechapishwa: 25/08/2021