Kujengea hoja juu ya makadirio hakumpi mtu udhuru wowote. Allaah (´Azza wa Jall) ametubainishia kheri na shari na hivyo hakuna udhuru wowote. Watu wanatumbukia katika mashaka kwa sababu ya kupekua mambo ambayo hayawahusu. Wanasema kuwa ikiwa Allaah amewaandikia kuingia Peponi basi wataingia na ikiwa wameandikiwa kuingia Motoni wataingia na hivyo hawahitaji kufanya chochote katika matendo. Tatizo ni kwamba hawatendei kazi fikira hiyo juu ya nafsi zao wenyewe. Kwa nini usiketi nyumbani na ukaacha kutafuta riziki na ukafikiria kuwa riziki itakukuta nyumbani ikiwa Allaah amekwishakuandikia nayo? Au badala yake utatoka na kupambana na kutafuta riziki? Hata wanyama hawakai na kusubiri chakula katika nyumba zao. Bali wanatoka na kwenda kutafuta riziki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Lau mgemtegemea Allaah ukweli ipasavyo basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege. Wanaruka wakiwa hawana kitu tumboni na wanarudi matumbo yao yakiwa yamejaa.”[1]
Allaah amemuumba mnyama katika maumbile ya kutafuta riziki na kufanya sababu. Tusemeje juu ya binadamu mwenye akili? Isitoshe, endapo mtu atakuibia kitu, je, utasema kuwa ndivo alivyopanga na kukadiria Allaah au utamshtaki? Utamshtaki na wala hutojengea hoja ya mipango na makadirio.
[1] at-Tirmidhiy (2344) ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 108-109
- Imechapishwa: 29/10/2024
Kujengea hoja juu ya makadirio hakumpi mtu udhuru wowote. Allaah (´Azza wa Jall) ametubainishia kheri na shari na hivyo hakuna udhuru wowote. Watu wanatumbukia katika mashaka kwa sababu ya kupekua mambo ambayo hayawahusu. Wanasema kuwa ikiwa Allaah amewaandikia kuingia Peponi basi wataingia na ikiwa wameandikiwa kuingia Motoni wataingia na hivyo hawahitaji kufanya chochote katika matendo. Tatizo ni kwamba hawatendei kazi fikira hiyo juu ya nafsi zao wenyewe. Kwa nini usiketi nyumbani na ukaacha kutafuta riziki na ukafikiria kuwa riziki itakukuta nyumbani ikiwa Allaah amekwishakuandikia nayo? Au badala yake utatoka na kupambana na kutafuta riziki? Hata wanyama hawakai na kusubiri chakula katika nyumba zao. Bali wanatoka na kwenda kutafuta riziki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Lau mgemtegemea Allaah ukweli ipasavyo basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege. Wanaruka wakiwa hawana kitu tumboni na wanarudi matumbo yao yakiwa yamejaa.”[1]
Allaah amemuumba mnyama katika maumbile ya kutafuta riziki na kufanya sababu. Tusemeje juu ya binadamu mwenye akili? Isitoshe, endapo mtu atakuibia kitu, je, utasema kuwa ndivo alivyopanga na kukadiria Allaah au utamshtaki? Utamshtaki na wala hutojengea hoja ya mipango na makadirio.
[1] at-Tirmidhiy (2344) ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 108-109
Imechapishwa: 29/10/2024
https://firqatunnajia.com/94-kulaumu-makadirio/