Miongoni mwa sifa za Allaah ni utambuzi. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) anajua ni watu wangapi wataingia Peponi na ni watu wangapi wataingia Motoni – aliyajua hayo tangu hapo kitambo kwa ujuzi Wake wa milele. Yale ambayo Allaah (Ta´ala) ameyakadiria hakutozidishwa juu yake wala kupunguzwa. Miongoni mwa hayo ni kwamba anajua ni watu wangapi wataingia Peponi na ni watu wangapi wataingia Motoni ni yepi watayoyafanya. Tunayaamini hayo na tunafanya matendo. Hatujadili juu ya mipango na makadirio. Hatuulizi vipi, kwa nini, vipi atafanyiwa hesabu juu ya kitu alichokadiriwa na maswali mengine kama hayo ambayo ni kupoteza tu wakati. Maswali kama hayo ni kupingana na Allaah (´Azza wa Jall). Kilicho cha wajibu kwako ni kumtii Allaah na kujiepusha na maasi. Sio kazi ya mja kupekua siri ya Allaah (´Azza wa Jall) na kugombana na Mola (Jalla wa ´Alaa). Kazi ya mja anachotakiwa ni yeye kufanya matendo. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walisema:
“Ee Mtume wa Allaah! Yale tunayofanya yamekwishapangwa au hayajapangwa?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Yamekwishapangwa.” Maswahabah wakasema: “Si tutegemee basi tuliyoandikiwa na tuache kutenda?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Fanyeni matendo! Kwani hakika kila mmoja ni mwenye kufanyiwa wepesi juu ya kile alichoumbiwa.”[1]
Allaah (Ta´ala) amesema:
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ
“Basi yule anayetoa na akamcha Allaah na akasadikisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi.”[2]
Sababu inatokamana na mja mwenyewe na makadirio yanatokamana na Allaah:
وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ
”Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza na akakadhibisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.”[3]
Kinachotakikana kwetu ni sisi kufanya matendo mema na kujiepusha na matendo maovu.
[1] al-Bukhaariy (4949) na Muslim (2647).
[2] 92:5-7
[3] 92:8-10
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 107-108
- Imechapishwa: 29/10/2024

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 107-108
Imechapishwa: 29/10/2024
https://firqatunnajia.com/93-kupingana-na-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)