94. Barzakh ni nyumba kati ya nyumba mbili

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ

”Nyuma yao kuna kizuzi mpaka siku watakayofufuliwa.” 23:100

Barzakh ni jina la kituo kati ya duniani na Aakhirah. Aayah hii inathibitisha hivo. Katika Barzakh watu wake wana mawasiliano na duniani na Aakhirah. Adhabu na neema ya kaburi ni adhabu na neema katika Barzakh. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameumba nyumba tatu; duniani, Barzakh na milele. Amefanya kila nyumba ina hukumu zake maalum. Amemfungamanisha mwanaadamu na kiwiliwili na roho. Katika dunia hii hukumu zinahusiana na viwiliwili ilihali roho ni zenye kufuata hivyo viwiliwili. Ndio maana hukumu za Kishari´ah zinatendewa zile harakati za nje ambazo mwanaadamu anadhihirisha hata kama ndani ya nafsi kutakuwa hakuafikiani na ule uinje wake.

Katika Barzakh hukumu zinahusiana na roho ilihali viwiliwili ni vyenye kufuata roho hizo. Kama jinsi roho zilikuwa ni zenye kufuata viwiliwili katika neema na adhabu za duniani, viwiliwili ni vyenye kuifuata roho katika neema na adhabu ya Barzakh. Katika Barzakh roho ndio zinazochukua nafasi ya mbele katika kuhisi neema na adhabu. Halafu zinenda mpaka kwenye viwiliwili. Katika dunia hii wiliwili ndivyo vinavyochukua nafasi ya mbele katika kuhisi neema na adhabu. Halafu zinaenda mpaka kwenye roho. Katika dunia hii viwiliwili viko dhahiri na roho zimejificha. Ukitaka kuyajua hayo mtazama anayelala hapa duniani. Ima anastarehe usingizini au anaadhibiwa. Roho ndio yenye kuhisi yote hayo ingawa mwili pia ni wenye kuifuata. Wakati mwingine taathira kwenye kiwiliwili inaweza kuwa ni yenye nguvu kabisa mpaka ikaonekana. Haya – na Allaah ndiye anajua zaidi – yanaonekana na watu wengi usingizini. Shaykh Nusayr al-Maqdisiy amenieleza:

“Nyusiku tatu niliota usingizini jinsi watu wanavyonitumia kama mfanya kazi. Niliwaogopa sana na nikafanya kazi. Nilipoamka nikahisi nimechoka kwelikweli.”

Akanambia nitazame mikono yake. Nilipotazama mikono yake nikaona malengelenge makubwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 204
  • Imechapishwa: 06/12/2016