94. Athar ”Allaah (´Azza wa Jall) kumswalia ni kule… ”

95 – Naswr bin ´Aliy ametuhadithia: Khaalid bin Yaziyd ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ja´far, kutoka kwa ar-Rabiy´ bin Anas, kutoka kwa Abul-´Aaliyah, ambaye amesema kuhusiana na Aayah:

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ

“Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Mtume.”[1]

”Allaah (´Azza wa Jall) kumswalia ni kule kumsifu na Malaika kumswalia ni kule kumuombea du´aa.”[2]

[1] 33:56

[2] Cheni ya wapokezi ni nzuri. Wapokezi wake ni waaminifu isipokuwa tu Abu Ja´far ar-Raaziy, ambaye kuna makinzano juu ya jina lake. Ana unyonge kutokana na kumbukumbu yake mbaya. Kwa ajili hiyo mtu anatakiwa kuwa makini juu ya yale anayosimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini katika hali kama hii hapana vibaya – Allaah akitaka. Pengine ndio sababu ya al-Bukhaariy alithibitisha kuwa kweli Abul-´Aaliyah amesema hivo. Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Ameipokea Ibn Abiy Haatim kupitia kwa Aadam bin Abiy Iyaas: Abu Ja´far ar-Raaziy na Khaalid bin Yaziyd al-´Atakiy wametuhaidthia.” (Fath-ul-Baariy (8/409))

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 82
  • Imechapishwa: 14/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy